Featured Kitaifa

ILEMELA YANG’ARA TUZO ZA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA AFYA NA ELIMU MKOA WA MWANZA

Written by mzalendoeditor
Wilaya ya Ilemela imeibuka kidedea katika tuzo za usimamizi bora wa miradi ya afya na elimu zilizotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel kwa wilaya zote za mkoa  huo.
Wilaya ya Ilemela imefanikiwa kutwaa tuzo ya usimamizi bora wa miradi ya afya kwa kuwa mshindi wa kwanza, tuzo ya mshindi wa pili mitihani ya kidato cha pili kitaifa kwa mwaka 2021, tuzo ya mshindi wa kwanza mitihani ya kitaifa kwa darasa la nne kwa mwaka 2021 ambapo mkuu wa mkoa wa Mwanza akazitaka halmashauri zote za mkoa huo kuweka msukumo katika kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi ya maendeleo Kwa wananchi sambamba na matumizi sahihi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla ameshukuru Kwa wilaya yake kufanikiwa kutwa tuzo hizo huku akiahidi kuongeza kasi katika kuisimamia wilaya yake katika kutekeleza miradi yenye tija Kwa wananchi itakayozingatia mahitaji ya wakati na thamani ya fedha
Zoezi la utoaji wa tuzo hizo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza wakiwepo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mameya na wenyeviti wa halmashauri.

About the author

mzalendoeditor