Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUZINDUA ROYAL TOUR JIJINI ARUSHA APRIL 28

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo(Happy Lazaro)
………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Royal Tour jijini Arusha April 28 mwaka huu 
Mkuu wa mkoa Arusha, John Mongella ametoa taarifa hiyo leo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha,(AICC).
Mongella amesema Rais Samia anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro asubuhi April 28 na baadaye uzinduzi utafanyika mchana kituo cha mikutano cha Arusha (AICC).
Amesema uzinduzi wa filamu hiyo unatarajiwa kuongeza idadi kubwa ya watalii nchini kwani sasa imekuwa gumzo kubwa duniani.
“Tunatarajia watalii kuendelea kuongezeka zaidi kutokana na kazi nzuri ambayo alifanya Rais kuongoza filamu hiyo”amesema
Amesema idadi ya watalii  imeanza kuongezeka  nchini baada ya uviko-19 mwaka 2020 walikuwa  620,867 na wameongezeka hadi 922,692 mwaka 2021.
Mongella amesema watalii wa ndani pia wameongeza kutoka 562,549 mwaka 2020 hadi kufikia 788,933.
Amesema uzinduzi wa kwanza ulifanyika jiji la NewYork April 18 na baadaye Aprili 21 jiji la Los Angeles  nchini Marekani.
Akizungumzia uzinduzi wa Arusha, Mkurugenzi wa mikutano na masoko wa AICC, Mkunde Mushi amesema wamejiandaa vizuri katika kufanikisha uzinduzi huo.

About the author

mzalendoeditor