Featured Kitaifa

KINANA ATEMBELEA KITUO CHA UKOMBOZI WA AFRIKA ,ATAKA WANANCHI KUJUA HISTORIA

Written by mzalendoeditor

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa ameongozana na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mohamed Mchengerwa (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara hiyo, Boniface Kadili alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya vifaa mbalimbali Vilivyotumika wakati wa Harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Boniface Kadili huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya  Maeneo mbalimbali ya Ukombozi wa Afrika nchini Tanzania   kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Boniface Kadili huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo na kuzungumzia  picha mbalimbali za  Urithi wa Utamaduni na huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahi pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamadudi, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakisoma Chapisho la Hotuba Mbalimbali za Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere alipotembelea maktaba ya wapigania ukombozi Kusini mwa Afrika, alipotembel alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.

*************************

 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema Chama kinaunga mkono juhudi na malengo ya serikali katika kuenzi, kutunza na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika.
 
Aidha, amewaomba Watanzania kutembelea kituo cha historia ya ukombozi kilichopo Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujua kazi kubwa iliyofanywa na wapigania uhuru na wana ukombozi wa Afrika, huku Tanzania kikiwa kitovu cha harakati hizo.
 
Kinana aliyasema hayo Leo, alipotembelea ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha majengo yake na kutunza kumbukumbu muhimu.
 
“Ukombozi wa Afrika walioshiriki ni wengi, nchinyi zilitoa michango kwa namna mbalimbali, lakini shgughuli zote hizi ziliongozwa na mtu mmoja bingwa wa mikakati anaitwa Mwalimu Julius Nyerere. katika Ziara hiyo aliambatana na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamadudi, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu.

About the author

mzalendoeditor