Na Amiri Kilagalila, Njombe.
Kijana ambaye hajafahamika haraka jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30 mkazi wa Igoma halmashauri ya mji wa Njombe amenusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage mara baada ya kukamatwa akiwa ameiba vitu mbali mbali Ikiwemo TV,Godoro,Blanketi na Mtungi mdogo wa gesi.
Luo Lameck Mgeni ni mzee aliyekuwa amempangisha awali katika nyumba yake kabla ya kumfukuza kutokana na tabia ya wizi anasema anashangaa kuona kijana huyo ameondoka kwake lakini amerudi na kuiba kwenye moja ya nyumba ya familia yake.
“Leo nikasikia kule nyumbani wameboboa nikauliza wameiba nini,kuingia mle ndani tukaona tandiko halipo na vitu vingine amechana chana ameweka nje”alisema Mzee Mgeni
Hata hivyo kabla kijana huyo hajafikiwa na hali mbaya kutokana na kipigo,Polisi imefika na kufanikiwa kumuondosha katika eneo hilo.