Featured Kitaifa

WATUHUMIWA 176 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI PWANI

Written by mzalendoeditor
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI  la Polisi Mkoa Pwani limekamata watuhumiwa 176  ambapo kati Yao 45 ni wahamiaji haramu.
Aidha Jeshi hilo limejipanga kukabiliana na matukio ya kiuhalifu pamoja  na uvunjifu wa amani katika kipindi hiki Cha sikukuu ya Pasaka na kuelekea kwenye Eid Al fitri.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,ACP Pius Lutumo alibainisha kwamba, jeshi hilo kupitia taarifa za kiintelijensia linaendelea na operesheni mbalimbali za kuzuia na kupambana na uhalifu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa hao na vifaa mbalimbali vya wizi.
“Vifaa tulivyovikamata Ni vya ujenzi, gongo ,bhangi ,Televisheni, magari, pikipiki, simu za mikononi,, Watuhumiwa wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.:;
Pamoja na hayo ,Lutumo alifafanua,kuelekea sikukuu ya Pasaka na Eid Al fitri vijana wengi hupenda kwenda sehemu za starehe na kutumia madawa ya kulevya na vilevi kupitiliza.
Aliwaasa wazazi wawe makini na kujiridhisha ili kujiepusha na ajali za barabarani na madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya ama vilevi.
Vilevile,Lutumo aliwataka wenye kumbi za starehe lazima waweke Utaratibu mahususi juu ya ulinzi wa watoto na Usalama wao endapo kutakuwa na disco toto.
 
Hata hivyo , Kamanda huyo alieleza, wanaendelea na ukaguzi wa magari katika road block na doria kali zitafanywa kwenye fukwe ambako watumiaji wa madawa ya kulevya,vilevi hujificha.
Lutumo alitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria zote za usalama 
barabarani na matumizi sahihi ya alama za barabarani ili kuepusha ajali,;:Na kwa wamiliki wa vyombo vya moto wakikishe vyombo Vyao ni vizima na vipo salama kwa matumizi.

About the author

mzalendoeditor