Featured Kitaifa

CHIKOTA ASHAURI MASOKO KUJENGWA MAENEO YENYE WATU

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna-DODOMA

Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota ameshauri masoko yajengwe kwenye maeneo yenye watu ili miradi hiyo iwe na tija kwa wananchi.

Chikota ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa mwaka 2022/23.

“Kwa kaka angu Mtenga limejengwa pale soko Chuno la fedha nyingi lakini kuna mgogoro wa wafanyabiashara kwenda kwenye lile soko kwenye maeneo mapya tusiruhusu suala kama hilo,”amesema.

Kuhusu uhaba wa walimu, amesema kuna tatizo kubwa la uhaba wa walimu ambapo ili mwalimu afundishe vizuri kwa kiwango kilichopo ni wanafunzi 45 kwa mwalimu mmoja na kwamba darasa la wanafunzi 60 halifundishiki.

“Lazima tutoe kibali maalum cha kuajiri walimu wetu ili elimu yetu iboresheke,”amesema.

Akizungumzia  mradi wa uboreshaji miundombinu kwenye Majiji (TACTIC), Chikota amepongeza kuongezwa kwa kasi ya mazungumzo ili uanze kutekelezwa.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuingiza Mji wa Nanyamba katika mradi huu tupo kwenye Miji 45 na tunasubiri sana kwa hamu nikuombe Waziri tusifanye makosa yaliyopita huko nyuma miradi hii tujenge kulingana na mahitaji ya sasa, Rais ameelekeza masoko yafuate watu na sio watu wafuate masoko,”amesema

About the author

mzalendoeditor