Featured Kitaifa

RAIS SAMIA MGENI RASMI MEI MOSI,RC MTAKA AWAITA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizindua ‘hashtag’ ya #MEIMOSI2022DODOMA KIVINGINE itakayotumika katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pochani) wakati akitoa taarifa ya Mkoa wake kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa  maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Meneja wa Biashara Kanda ya Kati Benki ya CRDB Jane Maganga ,akizungumza mara baada ya uzinduzi wa ‘hashtag’ ya #MEIMOSI2022DODOMA KIVINGINE itakayotumika katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya,akizungumza mara baada ya uzinduzi wa ‘hashtag’ ya #MEIMOSI2022DODOMA KIVINGINE itakayotumika katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  ‘hashtag’ ya #MEIMOSI2022DODOMA KIVINGINE itakayotumika katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

…………………………………………..

Na Bolgas Odilo-DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hasan,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa leo April 14,2022 jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati  akitoa taarifa kwa  waandishi wa  habari  pamoja na kuzindua ‘hashtag’ ya #MEIMOSI2022DODOMA KIVINGINE itakayotumika kwenye maadhimisho hyo.

Amesema kuwa  mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa sherehe za Mei Mosi kitaifa ambapo maadhimisho hayo yatakuwa tofauti na miaka iliyopita.

”Nataka  wakazi wa jiji la Dodoma pamoja na wilaya jirani kutumia fursa ya kufanya biashara ili kujiingizia kipato katika maadhimisho hayo”amesema RC Mtaka

Mtaka, amesema wiki ya maandalizi ya Mei Mosi mwaka huu yataanza rasmi Aprili 16, hadi 30 mwaka huu ambapo kilele itakuwa tarehe 1,Mei 2022.

“Katika kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha kila fursa inayojitokeza inachangia ujenzi wa uchumi imara,uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau ,umeazimia kutumia fursa ya Mei Mosi kitaifa kuziunganisha sekta zote za kiuchumi kwa manufaa mapana.

Hata hivyo Mtaka amesema  kuwa kutakuwa na michezo itakayochezwa katika mashindano hayo ni Mpira wa Miguu,Mpira wa Pete,Kuvuta Kamba,Kufukuza Kuku,Draft,Bao na Riadha.

“Tutatumia viwanja vya Jamhuri,Chuo cha St John,Kilimani Veterani,Shell- Wajenzi.Chinangali Park.Vijana na Mtekelezo.Shughuli hii ni yetu sote  tutumie fursa hii kuwakaribisha katika mashindano yetu haya tutashirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA),Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wadau kuhakikisha sherehe hizi zinafanikiwa,”amesema.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema wamejipanga kuhakikisha sherehe za mwaka huu zinakuwa na ubora ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga sherehe hizo Mei mosi mwaka huu.

Amesema sherehe  hizo zitaambatana na maonesho ambayo yatawashirikisha wajasiriamali wadogo pamoja na wa kati,Taasisi za umma na za huduma,wafanyakazi wakati na wakubwa,Taaisi za fedha,viwanda,vyama vya wafanyakazi na Wizara.

Naye Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Kati, Jeni Maganga amesema hiyo ni fursa nzuri na itasaidia kuwaanda wafanyabiashara kuweza kujitegemea na kujiinua kiuchumi ambapo amedai wameandaa fursa nzuri ya mikopo kwa watanzania.

Mratibu wa Mei Mosi mwaka huu,kutoka Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (TUCTA),Wandiba Kongoro  amesema maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yamekamilika na timu 28  zitashiriki  huku akiwaomba wakazi wa Dodoma kujitokeza katika viwanja mbalimbali kwa ajili ya kuangalia michezo mbalimbali.

About the author

mzalendoeditor