Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne Muliro
…………………..
NA MUSSA KHALID
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja aitwaye Latifa Bakari (33),kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne.
Akitoa tarifa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam,Kamanda wa Jeshi hilo Muliro Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyo mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa hayo baada ya kumpiga kupita kiasi.
Aidha Kamanda Muliro amesema Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumi huyo 06/4/mwaka huu aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu),kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la RiverSide UBUNGO.
‘Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa tarifa Polisi,Polisi ilimuhoji kwakina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwa onesha Polisi mwili wamtoto huyo ulipokuwa’amesema Kamanda Muliro
Kamanda huyo ameendelea kueleza kuwa Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi limewakamata watu wanne(4) akiwemo Omary Ally mkaziwaTegeta na mwezake Juma Sulleiman, mkazi waWazo na wanunuzi wavifaa hivyo Amos John,mkazi waTegeta na Mokolo Machage,kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu miundombinu ya Shirika la UmemeTanesco ikiwemo Nyaya aina ya Copper kwa lengo la kuziuza.
Jeshi hilo limeendelea kutoa onyo kali kuwa halita mvumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma na atakayejaribu atakamatwa na mifumo ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria itazingatiwa.