Featured Michezo

SIMBA YAZIDI KUPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA WA LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna

MABINGWA Watetezi Simba wamezidi kupunguzwa kasi katika mbio za ubingwa baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 41 nafasi ya pili huku Polisi Tanzania wanabaki nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 24.

Sasa Simba wamezidiwa Pointi 10 na Yanga wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na  Pointi 51 huku kila  timu ikicheza mechi 19.

About the author

mzalendoeditor