Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula, Aprili 9, 2022 ameshiriki ibada ya misa takatifu ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi, Mabughai Aidan Rwegoshora Felix.

Ibada hiyo ya misa imefanyika katika Parokia ya Unga Limited, Tengeru Jimbo Kuu Katoliki la Arusha ikiongozwa na Padre Festus Mangwige, Paroko wa Parokia hiyo.

Aidha, ibada imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo pamoja na watumishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.

Katika ibada hiyo, Padre Mangwige ametumia sehemu ya familia yake kumfariji Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula na viongozi wengine wa Wizara kutokana na vifo vya wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (CDTI) Monduli Elibariki Martin Ulomi na cha Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi, Mabughai Aidan Rwegoshora Felix.

Mara baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu Aidan Rwegoshora Felix umesafirishwa kuelekea Mabughai kwa taratibu nyingine za kuagwa na kisha baada ya hapo utasafirishwa kuelekea Muleba, mkoani Kagera kwa mazishi.

Marehemu Aidan Rwegoshora Felix aliaga dunia ghafla Aprili 7, 2022 katika hospitali ya wilaya ya Monduli.

Previous articleWAZIRI MHAGAMA ATETA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI
Next articleMWANAUME WA MIAKA 26 MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MWAKA MMOJA SHINYANGA MJINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here