Featured Kitaifa

WAZIRI MHAGAMA ATETA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini chenye lengo la kuwafahamisha  kuhusun mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha utumishi wa umma leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Joyce Ndalichako ,akizungumza kwenye kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini  leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

NAIBU Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daudi,akielezea lengo la kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini  leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali  wakati wa kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini chenye lengo la kuwafahamisha  kuhusun mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha utumishi wa umma leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

………………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amekutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini kwa lengo la kuwafahamisha  kuhusun mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha utumishi wa umma.

Akizungumza leo April 9,2022 jijini Dpodoma wakati wa kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuhusu mtazamo wa serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha utumishi wa umma, uwajibikaji wa hiari na matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa watumishi wa umma.

Waziri Mhagama amesema kuwa  ili kupata mfumo sahihi wa kupima utendaji kazi wa Watumishi wa Umma na taasisi kama ilivyoelekezwa na Rais Samia.

“Ndio maana Ofisi yangu tumepokea maelekezo ya Rais ya kuihakikisha tunaweka mifumo imara itakayotuwezesha pia kufikia mipango mbalimbali ya maendeleo kutokana na utendaji mzuri kwa watumishi wa umma.”amesema

Amesema Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) unatarajiwa kuanza kazi Mwezi Julai mwaka huu ili kuondokana na kero za usimamizi wa utendaji kazi zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa awali wa OPRAS, ambao haukuakisi hali halisi ya utendaji kazi wa watumishi hali iliyoleta hisia za kupendeleana au kuoneana.

“Mfumo mpya wa PEPMIS utakuwa ni wa kielektroniki na utaondokana na matumizi ya makaratasi,pia utaongeza uwazi katika usimamizi wa watumishi na kuondoa upendeleo na uonevu katika upimaji wa utendaji wa watumishi,pia mfumo huu pia utahamasisha uwajibikaji wa hiari na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za utendaji kazi wa watumishi.”amesema Waziri Mhagama

Aidha amesema kuwa Ofisi yake imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao na kujenga mifumo ya TEHAMA inayohusu uendeshaji wa Serikali wa kila siku na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa umma.

Mhagama amesema,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imefanikiwa kujenga Mfumo wa Sema na Waziri , Mfumo wa e-mrejsho, Mfumo wa Dawati la Huduma kwa Mteja maarufu kama UTUMISHI Call Centre ,Mfumo maalum wa Tathmini ya hali ya Mfumo wa Huduma Mtandao kwa Watumishi (Watumishi Portal).

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu)  Joyce Ndalichako amesema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kupima utendaji kazi serikalini  Rais amelekeza ushirikishwaji wa Vyama vya Wafanyakazi ili waendelee  kuwa daraja kati ya waajiri na Wafanyakazi kwa kuchochea na kuhimiza utamaduni kwa Wafanyakazi kudai haki na kutimiza wajibu wao.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu imeendelea kutekeleza maagizo ya  Rais kwa kukamilisha Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji wa Vibali vya Kazi kwa raia wa kigeni ambao  umepunguza muda wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi kutoka siku za kazi 14 hadi siku 7.

Naye  Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) Deus Seif ,ameishukuru serikali kwa kuja na mfumo huo mpya ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza changamoto kwa watumishi wa umma.

“Mfumo wa awali wa OPRAS uligubikwa na malalamiko mengi kwa kuwa ulikuwa hautendi haki kwa watumishi katika kupatiwa stahiki na masuala mbalimbali ikiwemo hatua zinazochukuliwa kwa mtumishi pale anapokuwa amekiuka maadili ya utumishi,”amesema

About the author

mzalendoeditor