Featured Kitaifa

MWANAUME WA MIAKA 26 MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MWAKA MMOJA SHINYANGA MJINI

Written by mzalendoeditor
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Ndala Mjini Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa Mwaka mmoja na miezi 11.
Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Ijumaa Aprili 8,2022 majira ya saa nane na nusu mchana.
 
“Tunamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11”,amesema Kamanda Kyando.
“Mtoto huyo alibakwa na baba yake wa kambo wakati mama wa mtoto huyo akiwa ameenda dukani. Mtuhumiwa amemuoa huyo mama akiwa tayari ana mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Kyando.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda unyama huo alimpeleka mtoto huyo kwa mama mwenye nyumba kisha kumwambia kuwa mtoto huyo anatokwa damu kwa sababu amejikata kisu.

About the author

mzalendoeditor