Featured Kitaifa

WAZIRI DKT GWAJIMA:’TUTASHIRIKIANA NA BALOZI ZETU KUFIKISHA FURSA ZA MASOKO KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE’

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM- Berlin Ujerumani

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima amesema Wizara yake itashirikiana Balozi zilizopo katika nchi mbalimbali duniani ili kutumia fursa zilizopo katika nchi hizo ikiwemo masoko kwaajili ya bidhaa za wajasirimali Wanawake jamii ya Watanzania kwa ujumla.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo Aprili 09,2022 jijini Berlin nchini Ujerumani mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa G7 uliokwenda kuwawezesha wajasirimali hasa Wanawake katika kuendeleza bishara zao kwa kupata masoko ya Kimataifa.

Dkt. Gwajima amewapongeza wakina mama kutoka Tanzania walioshiriki kwenye maonesho ya bidhaa za mbogamboga …
[8:46 pm, 09/04/2022] Kuni_Afya: TUTASHIRIKIANA NA BALOZI ZETU KUFIKISHA FURSA ZA MASOKO KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE- DKT. GWAJIMA

Na WMJJWM- Berlin Ujerumani

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima amesema Wizara yake itashirikiana Balozi zilizopo katika nchi mbalimbali duniani ili kutumia fursa zilizopo katika nchi hizo ikiwemo masoko kwaajili ya bidhaa za wajasirimali Wanawake jamii ya Watanzania kwa ujumla.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo Aprili 09,2022 jijini Berlin nchini Ujerumani mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa G7 uliokwenda kuwawezesha wajasirimali hasa Wanawake katika kuendeleza bishara zao kwa kupata masoko ya Kimataifa.

Dkt. Gwajima amewapongeza wakina mama kutoka Tanzania walioshiriki kwenye maonesho ya bidhaa za mbogamboga na matunda na kuwaomba kuwashirikisha Wanawake wengine wa Tanzania kwa lengo la kupanua wigo wa upatikanaji wa masoko ya bidhaa hasa masoko ya Kimataifa.

Aidha Dkt. Gwajima amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Abdallah Posi kwa maandalizi mazuri na mapokezi mazuri waliyoyapata wakati wa Mkutano wa G7.

“Tunamshukuru sana Mhe. Balozi Posi kwa maandalizi mazuri ambayo yamefanywa, lakini pia tunampongeza Balozi Hoyce Temu aliyesafiri kutoka Uswis hadi hapa Berlin kuja kuungana na wajasiriamali kutoka Tanzania walikuwa na Kampuni zaidi ya 12, hakika hili limeongeza nguvu na umuhimu wa Mkutano huu kwa Usatwi wa Wajasirimali Tanzania” alisema Dkt Gwajima

Amesisitiza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Balozi mbalimbali kote Duniani itahakikisha inashirikiana ili fursa za masoko na zingine zilizopo ziweze kuwafikia Wanawake wa Tanzania na jamii kwa ujumla.

“Tumejifunza na kuona fursa zilizopo huku Ujerumani na nchi zingine zote zinashirikiana na Tanzania kupitia ubalozi wetu na niahidi kutumia tuliyojifunza kutokana na mkutano huu wa G7 kwa Wanawake wa Tanzania na jamii kwa ujumla” alisema Dkt. Gwajima.

Akiwa katika Mkutano wa G7 Waziri Dkt. Gwajima alitembelea mabanda ya watanzania wakiwa kwenye maonesho ya Berlin Messe nchini Ujerumani ambayo yalishirikisha wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kutoka Arusha, Njombe na Iringa.

Mkutano huu wa G7 umefanyika jijini Berlin nchini Ujerumani kuanzia April 06- 09,2022 ulilenga uzingatiaji wa mchango wa wanawake wanaofanya kazi za nyumbani na kazi za huduma zisizo na ujira ingawa zina mchango mkubwa katika ustawi wa jamii na pato la nchi.

About the author

mzalendoeditor