Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
 
Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa mambo ya Nje kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba. Kushoto mwa Bw. Grolig ni maafisa alioambatana nao kutoka Jamhuri ya Czech.
…………………………………………………..
Na Mwandishi wetu, Dar
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
 
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya Czech katika sekta za biashara na uwekezaji, kilimo, elimu na teknolojia.
 
Balozi Mulamula aliwakaribisha wawekezaji kutoka Czech kuwekeza nchini pamoja na kutia mkazo wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Czech.
 
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech, Bw. Grolig amesema ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Czech kuja kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama ya kuwekeza.
 
“Jamhuri ya Czech imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na katika kutimiza azma hiyo, wafanyabiashara na wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza ndege ndogondogo Pamoja na magari makubwa hapa Tanzania,” amesema Bw. Grolig
 
Pia ameongeza kuwa kwa sasa Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hapa nchini Tanzania ili kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi kuja Tanzania kutafuta fursa za uwekezaji,” amesema Bw. Grolig.
Previous articleSAGINI ATAKA WAKURUGENZI WAMILIKI WA MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI TANZANIA KUSHIRIKIANA.
Next articleNAIBU WAZIRI PINDA ATOA MAAGIZO KWA WAFANYAKAZI WA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here