Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI PINDA ATOA MAAGIZO KWA WAFANYAKAZI WA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda,akizungumza wakati akifungua baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 lililofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda,akifafanua jambo kwa washiriki wakati akifungua baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 lililofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Wakili Mkuu wa Serikali Boniface Luhende,akitoa taarifa wakati wa kikao cha Baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 lililofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda (hayupo pichani) wakati wa kikao cha  Baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 Kilichofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi mara baada ya kufungua Baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 lililofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari  mara baada ya kufungua Baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 lililofanyika leo April 8,2022 jijini Dodoma.

…………………………………………

Na Bolgas Odilo-DODOMA

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Geofrey Pinda,amesema ni wajibu wa kila mtumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  kuhakikisha anafahamu wajibu wake mahali pa kazi, ili aweze kutekeleza malengo aliyopangiwa na kuhakikisha anayakamilisha katika muda uliopangwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo,Aprili 8,2022 jijini Dodoma wakati akifungua baraza la pili la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2021/22 ,Mhe.Pinda amesema kila mtumishi ahakikishe anatunza mali na vifaa alivyokabidhiwa kufanyia kazi, Wajibu huo ni pamoja na kuwahi kazini.

“Hivyo, ni wajibu wa kila mtumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  kuhakikisha anafahamu wajibu wake mahali pa kazi, ili aweze kutekeleza malengo aliyopangiwa na kuhakikisha anayakamilisha katika muda uliopangwa,”amesema.

Kuhusiana na bajeti,Naibu Waziri huyo amesema anaamini Ofisi hiyo  itakuwa imeandaa bajeti yake kwa kufuata utaratibu wa Medium Term Expenditure Framework (MTEF).

“Utaratibu ambao bajeti huandaliwa kulingana na mipango iliyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa taasisi husika kwa kuzingatia vyanzo vya mapato na rasilimali zilizopo.Mtindo huu wa bajeti huonesha wazi wazi utendaji wa kila idara hususani kwa mtu mmoja mmoja kulingana na vipimo vya utendaji wake.

“Nichukue nafasi hii kuwataka wafanyakazi wa OWMS kufuata utaratibu unaoelekezwa na Bajeti yenu. Mtakapokuwa tunafanya mapitio ya Bajeti ya nusu mwaka hapo baadaye, tutaona ni nani au Idara gani haikufanya kazi kulingana na malengo ya OWMS,”amesema.

Pinda,amewahakikishia  wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa niaba ya Wizara wataendelea  kuwaunga mkono kwa kazi nzuri wanayoendelea  kuifanya licha changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.

“Changamoto zingine nimezichukua na tutazishughulikia kwa kushirikiana na viongozi wenzangu ikiwa ni pamoja na kuziwasilisha zile changamoto za kiutumishi ili ziweze kushughulikiwa kwa mujibu wa Utumishi wa Umma.

“Ni matumaini yangu mtalitumia Baraza hili kuhimiza kila mtumishi ajue wajibu wake wa kutumia muda wa kazi ipasavyo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha OWMS kusonga mbele katika kutekeleza maagizo ya serikali pamoja na kutoa huduma kwa wakati,”amesema.

Awali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Boniface Luhende, ,amesema kuwa katika kipindi cha utawala wa Serikali ya awamu ya Sita (Machi 2021 hadi Machi, 2022) Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali iliongezewa bajeti yake kutoka Shilingi Bilioni 11.48 kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 hadi Bilioni 12.13 kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 5.4.

“Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendesha mashauri ya madai 1,102 na ya Usuluhishi 117. Hivyo kufanya jumla ya mashauri yaliyoendeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuwa 1,219.

Aidha, mashauri ya madai yaliyomalizika hadi Januari 2022 na Serikali kushinda ni 444 na Mashauri ya Usuluhishi 6 na hivyo kuokoa kiasi cha Shilingi Bilioni 236.6.

Amesema Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeweza kujaza nafasi mbalimbali  za ajira.

“Ofisi ilipata vibali vya kuajiri watumishi 23 wapya, watumishi watatu  kwa nafasi ya ajira mbadala na mtumishi mmoja wa kuhamia. Tayari Ofisi imeweza kujaza nafasi hizo na kufikia watumishi 159,”amesema.

 

About the author

mzalendoeditor