Featured Michezo

LIVERPOOL YAIZAMISHA BENFICA UGENINI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Liverpool imeendeleza ubabe baada ya jana kuwachapa wenyeji, Benfica mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa da Luz Jijini Lisbon, Ureno.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Ibrahima Konate dakika ya 17, Sadio Mane dakika ya 34 na Luis Diaz dakika ya 87, wakati la Benfica lilifungwa na Darwin Nunez dakika ya 49.

About the author

mzalendoeditor