Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia,aakitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 3,2022 kuhusu kongamano la Kisayansi la Maji linalotarajia kufanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………..
MKUU wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia,amesema kuwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi anatarajiwa kuzindua Kongamano la Kisayansi la Maji linalotarajiwa kufanyikia kwa siku mbili kuanzia kesho April 4-5 mwaka huu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Hayo ameyasema leo April 3,2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kongamano hilo.
Dkt. Karia amesema wadau wa sekta ya maji zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki.’
‘Kongamano hilo linatarajiwa kuanza kesho April 4 na litazinduliwa na Mhe Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Maji na wadau wa sekta ya maji zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali watashiriki”amesema Dk.Karia
Aidha, matokeo ya tafiti zaidi ya 60 zenye lengo la kuleta matokeo chanya katika kutatua changamotop za sekta ya maji nchini zinatarajiwa kuwasilishwa.