RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameahidi kutoa Euro bilioni 20 sawa na Tsh. Trilioni 51 ili kudhibiti ongezeko la bei ya Umeme na Gesi
Rais Macron amesema hayo katika mkutano wa kwanza wa hadhara kabla ya kufanyika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa urais Nchini humo.
Ameahidi kuwapatia marupurupu yasiyokatwa kodi watumishi wa umma na kupambana na mfumuko wa bei.