Na Alex Sonna

SIMBA  na RSB Berkane zimetinga kibabe hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi katika mechi zao za mwisho Kundi D.

Simba akicheza uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wameichapa US Gendarmerie mabao 4-0 bao la kwanza likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 63.

Mabao mawili yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 huku bao la nne akijifunga mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu baada ya mpira kurudishiwa na beki wake.

Berkane nao wameifunga ASEC Mimosas bao 1-0 likipatikana dakika ya 28 likifungwa na Chadrack Lukombe kwa Mkwaju wa Penalti

Kwa ushindi huo Timu hizo zimemaliza zikiwa na Pointi 10 kila mmoja huku RSB Berkane wakiongoza wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa nafasi ya tatu ikishikwa na ASEC Mimosas  Pointi 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa pointi zao 5.

Previous articleMKUTANO WA DHARURA WA KAMATI YA MAWAZIRI WA SADC KUFANYIKA NCHINI AFRIKA KUSINI
Next articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRIL 4,2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here