Featured Kitaifa

WAZIRI NDUMBARO AKABIDHI VYETI YA UWEKEZAJI MAHI KWA KAMPUNI YA GRUMETI NA MWIBA HOLDINGS LTD, ATOA NENO KWA WAWEKEZAJI

Written by mzalendoeditor
  
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi  kwa wawekezaji  wa sekta ya utalii pamoja na kuendelea kuboresha  huduma za kitalii nchini ikiwemo upatikanaji wa leseni ya shughuli za utalii kwa uharaka zaidi pamoja na mifumo ya malazi.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kutoa fursa katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje ya nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi
Dkt.Ndumbaro amesema  hayo  leo Jijini Dares Salaam  wakati akikabidhi vyeti kwa wawekezaji waliokidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya uwekezaji mahiri katika maeneo ya Wanyamapori (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),ambao ni  kampuni mbili  za  Grumet  Services Ltd pamoja na Mwiba Holding LTD
Hivyo amewasisitiza wawekezaji wazawa pamoja na wa kigeni kulinda na kutangaza utalii na  maeneo ya uhifadhi na vivutio hapa nchini, katika maeneo waliyopewa kuwekeza kwa kushirikiana na serikali.
Pia Waziri Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji wa kigeni kuwekeza nchini, akiitaja Tanzania kuwa ni salama, yenye amani na demokrasia na kwamba Wizara anayoiongoza imefungua milango kwa wawekezaji wote kuja kuwekeza nchini.
“Sisi Kama Wizara ya Maliasili na Utalii, falsafa yetu ni moja tu, mteja ni mfalme. Ndio maana mimi, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, tuko tayari kukutana na mwekezaji wa aina yoyote yule, muda wowote ule kujadili changamoto zozote zile, milango iko wazi,”amesema.
Pamoja na hayo Dkt.Ndumbaro, ameipongeza TAWA kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa akisema kuwa Taasisi hiyo ni changa kuliko Taasisi zingine lakini wanafanya kazi ngumu na  mazingira magumu zaidi ila wanafanya vizuri.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TAWA,Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kuipatia TAWA fedha kiasi cha Shillingi Billioni 12.9, ili kutekeleza miradi ya miundombinu ya Utalii kupitia kampeni ya Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19.
Amesema miradi  hiyo inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye maeneo ya SWICA huku akithibitisha kuwa TAWA imeweka mipango madhuhuti, kuhakikisha miradi yote ambayo imekusudiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha hizo inatekelezwa ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora uliokusudiwa.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd, Mr Graham Ledger amesema kampuni ya Grumeti inashukuru kupata cheti cha umiliki wa Vitalu viwili kwa sasa na  inaahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kulina na kuendeleza shughuli za Uhifadhi nchini
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mark Ghaui ameishukuru Serikali kwa juhudi inazofanya kuhakikisha shughuli za Uhifadhi zinaleta tija kwa taifa  kwa kuhakikisha Uhifadhi unaimarika kwa kuleta faid ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi kwa kupitia uwekezaji huo wa muda mrefu
HAARI KATIKA PICHA
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( katikati)  akizungumza kabla ya  kukabidhi vyeti  kwa Makampuni ya Grumeti Reserves Ltd na Mwiba Holdings Ltd mara baada ya kukikidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya Uwekezaji Mahiri katika maeneo ya Wanyamapori  (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  Kushoto  Katibu Mkuu wa Maliasili na kushoto ni  Utalii, Dkt.Francis Michael akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA,  Meja Jenerali Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd, Mr Graham Ledger ( wa pili kushoto)  ambaye ni Mwekezaji aliyekidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya Uwekezaji Mahiri katika maeneo ya Wanyamapori  (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  Katikati ni Katibu Mkuu wa Maliasili na kushoto ni  Utalii, Dkt.Francis Michael akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Grumeti Reserves Ltd, Prof. Hussein Hassan Sosovele
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhi cheti kwa  Mwakilishi  wa Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, Abdulkadili Mohamed ambaye Kampuni yake imekidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya Uwekezaji Mahiri katika maeneo ya Wanyamapori  (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Maliasili na kushoto ni  Utalii, Dkt.Francis Michael akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mark Ghaui ( wa pilo kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedi Jenerali Hamisi Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akisaini vyeti kabla ya kukabidhi k kwa Makampuni ya Grumeti Reserves Ltd na Mwiba Holdings Ltd mara baada ya kukikidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya Uwekezaji Mahiri katika maeneo ya Wanyamapori  (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  Kushoto  Katibu Mkuu wa Maliasili na kushoto ni  Utalii, Dkt.Francis Michael akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA,  Meja Jenerali Semfuko

About the author

mzalendoeditor