Featured Kitaifa

KINANA ATEULIWA KUGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI CCM, MEMBE AREJESHEWA UANACHAMA

Written by mzalendoeditor

………………………….

Na Bolgas Matembo, Dodoma.

Kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi kimemteua Abdrahman Kinana kuwa mgombea wa kiti cha makamu mwenyekiti wa CCM , Bara.

Hayo yamesemwa mapema leo Alhaisi 31 Machi 2022 na katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Kinana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mzee Philip Mangula ambaye ameandika barua ya kung’atuka nafasi hiyo na kuipeleka kwa mwenyekiti wa CCM rais Samia Suluhu Hassan.

Pia Shaka amesema maandalizi ya mkutano mkuu huo maalumu yamekamilika na kwamba Mwenyekiti wa CCM ametembelea leo ukumbi huo na kuridhishwa na maandalizi yake.

Aidha, Shaka alisema kuwa Halmashauri kuu ya CCM Taifa imemsamehe na kumrudishia uanachama Bernard Membe baada ya kuandika barua za kuomba msamaha zaidi ya mara moja.

Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na alifukuzwa uwanachama tangu Februari 2020 kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Pia, aliwataka wajumbe wote wa CCM kuhudhuria mkutano mkuu maalumu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho Aprili Mosi 2022 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma

Katiba ya CCM ibara ya 100 toleo la mwaka 2020, Makamu mwenyekiti wa CCM inasema atachaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa.
Aidha mwenyekiti wa CCM Rais Samia amempongeza Mangula kwa utumishi wake uliotukuka katika CCM kwa muda mrefu.

About the author

mzalendoeditor