Featured Kitaifa

SHAKA:’CCM HAITOMBAGUA RAIA YEYOTE KATIKA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII’

Written by mzalendoeditor

Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa na wanachama wa CCM Mkoa wa Dodoma wakiwa katika maandamano ya amani yaliyofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM walioshiriki kwenye maandamano ya amani ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwakaribisha wajumbe wa CCM kutoka maeneo tofauti nchini yaliyofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde, akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM walioshiriki kwenye maandamano ya amani ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwakaribisha wajumbe wa CCM kutoka maeneo tofauti nchini yaliyofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

Baadhi ya Wasanii walioshiriki kwenye mapokezi ya Wajumbe wa CCM mkoani Dodoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde wakiwatazama wananchi waliokuwa wanaingia katika Viwanja wa Nyerere Square kwenye kuwapokea wajumbe wa CCM mkoani Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu Dodoma Mjini Mariam Ditopile (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka,(kulia) wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa CCM mkoani Dodoma ambayo yalifanyika kwa maandamano ya amani.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja kati ya wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi ya Wajumbe wa CCM mkoani Dodoma.

………………………………

Na Bolgas Odilo, Dodoma.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuendelea kutoa huduma zote za kijamii kwa wananchi wake bila kujali utofauti wa itikadi za vyama kwa kuwa ubaguzi sio msingi wa chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31,2022 jijini Dodoma na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM walioshiriki kwenye maandamano ya amani ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwakaribisha wajumbe wa CCM kutoka maeneo tofauti nchini.

“Chama hiki tangu kimezaliwa mwaka 1977 kutoka kwa vyama anzilishi TANU na ASP tulipitia katika nyakati tofauti tofauti za uongozi mpaka kufikia awamu hii ya sita lakini huko kote Chama hiki hakijapata kutoa huduma kwa misingi ya ubaguzi wa aina yeyote ile kwa sababu sio asili yetu.

“CCM chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan tutaendelea kutoa huduma za kijamii bila kujali itikadi ya mtu, ukabila kwasababu hiyo sio sera ya chama hiki.

“Kupitia awamu hii ya sita wasanii wameanza kupata mirabaha yao, hiyo ndiyo serikali ya Chama cha Mapinduzi na bado mambo mengine makubwa yanakuja,” alimalizia Shaka.

Kwa upande wake Mwenyeji wa Maandamano hayo Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde ameshukuru na kupongeza jitihada ambazo zinaendelea kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake.

“Dodoma tunamshukuru sana mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya hapa Dodoma, ametupa heshima kubwa sana na Dodoma inang’ara hivi sasa.

“Mheshimiwa Rais ametuletea Shilingi Bilioni 20 tunajenga barabara za lami ndani ya jiji la Dodoma kuanzia Shoppers Plaza mpaka stendi ya Job Ndugai lakini pia tunajengewa barabara ya mzunguko na mambo mengi yanakuja Dodoma.

“Tupo tayari kufanya nae kazi muda wowote na vijana wa Dodoma tuko tayari kwa jambo lolote kwaajili yakulinda Chama chetu na kumlinda Rais wetu,” alihitimisha Mavunde.

Nao wanachama pamoja na viongozi wa chama waliojitokeza kwenye mapokezi hayo hawakusita kuonesha uungaji mkono kwenye jitihada zinazoendelea kufanywa na Rais Samia.

About the author

mzalendoeditor