Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga Mei 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita

Katika kesi hiyo washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Tarehe hiyo imetajwa leo Alhamisi Machi 31, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo.

Amesema kwa kuwa watuhumiwa hao wapo mahabusu kesi hiyo itatajwa Aprili 13, 2022 kabla ya kutolewa hukumu Mei 31.

“Mshitakiwa wa tatu ambaye hajasaini nampa siku moja kufanya hivyo, kesho awe amesaini na iletwe mahakamani. Kesi itatajwa Aprili 13, kwa sababu washitakiwa ni mahabusu na hukumu itatolewa Mei 31, 2022” amesema.

Hata hivyo Askari Magereza, Inspekta Ramadhan Misanga ameieleza mahakama kuwa Watson Mwahomange ambaye ni mshtakiwa wa tatu aliyekuwa akijitetea mwenyewe baada ya aliyekuwa wakili wake kujitoa, hajaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa.

Aidha Hakimu Kisinda amemuongezea muda wa siku moja Mwahomange kuwasilisha hoja zake za majumuisho zikiwa zimesainiwa mahakamani hapo.

CHANZO:MWANANCHI

Previous articleSHAKA:’CCM HAITOMBAGUA RAIA YEYOTE KATIKA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII’
Next articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRIL 1,2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here