DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaagiza Makamanda wa Polisi nchi nzima kufanya operesheni ya mwezi mmoja ya kudhibiti makosa ya usalama barabarani ambayo kwa kipindi cha mwezi wa tatu mwaka huu yameonekeana kuongezeka.

IGP amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Rufiji ma RTOs na DTOs pamoja na Wakuu wa Operesheni kutoka kwenye mikoa hiyo.

Aidha, katika kikao kazi hicho IGP Sirro ametoa agizo kwa wananchi kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuepusha ajali zinazoweza kuepukia.

Katika hatua nyingine IGP Simon Sirro amekutana na kuzungumza na balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe. Hamdi Mansour Abuali aliyemtembelea ofisini kwake Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama na ushirikiano.

Previous articleASILIMIA NNE YA WATUMIA MITANDAO YA KIJAMII NI WAHANGA WA UKATILI MITANDAONI- DKT. CHAULA
Next articleKINABABA WATAKIWA KUONGOZANA NA WAKE ZAO KLINIKI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here