Featured Kitaifa

WANAWAKE WATATU WAUWA KWA KUCHOMWA MOTO TUHUMA ZA KUROGA MTU SINGIDA

Written by mzalendoeditor
Polisi na baadhi ya wanakijiji wakiwa eneo la tukio
**
Wanawake watatu wenye umri unaozidi miaka 80 wakazi wa kijiji cha Kisharita wilayani Iramba mkoani Singida wameuawa na wananchi, baada ya kuwatuhumu kuhusika na kifo cha Agnes Msengi mkazi wa kijiji hicho.
Kufuatia tukio hilo watu sita wanashikiliwa na polisi akiwemo Mwenyekiti na Afisa Mtedaji wa kijiji hicho cha Kisharita kilichopo wilayani Iramba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa baada ya kutokea kifo hicho cha Agnes, wananchi kwa kushirikiana na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji waliwakamata wanawake hao watatu na kuwafungia nyumbani kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho.
Inadaiwa kuwa mara baada ya kutoka kwenye mazishi, wananchi wakiongozwa na Mtendaji wa kijiji waliwahoji wanawake hao kuhusiana na kifo cha kabla ya kuwauwa kwa kuwachoma moto.
Via – EATV

About the author

mzalendoeditor