Featured Michezo

CAF YAIPIGA FAINI MILIONI 250 RSB BERKANE KWA KUFANYA FUJO DHIDI YA SIMBA

Written by mzalendoeditor

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeitoza faini klabu ya RSB ​​Berkane ya Morocco faini ya jumla ya dola za Kimarekani 108,000, zaidi ya Sh. 250 za Tanzania kwa kufanya vurugu kwenye mechi zote mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Simba.

Katika mechi hizo za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, nchini Morocco mashabiki wa Berkane waliwatupia vitu wachezaji wa Simba Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Februari 27, mwaka huu  wenyeji wakishinda 2-0 na kwa kosa hilo wametozwa faini ya dola 8,000.
Na kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba wakiibuka na ushindi wa 1-0 Machi 13, Makamu wa Rais wa Berkane, Majjid Madrane alivamia uwanjani na kuwaongoza wachezaji wake kuwafanyia fujo marefa.
Kwa kosa hilo, Kamati ya Nidhamu ya CAF kwanza imemfungia Madrane kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazotambauliwa na bodi hiyo ya kandanda barani kwa mwaka mmoja pamoja na kumpiga faini ya dola za Kimarekani 100,000.

About the author

mzalendoeditor