Featured Kitaifa

RC MTAKA AWAASA WALEZI WA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA MASHULENI KUSIMAMIA KWA WELEDI NA KUELIMISHA WANAFUNZI

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,akizungumza  wakati akifungua Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,akieleza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

MKUU  wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo,akizungumzia lengo la semina hiyo wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

KAMISHNA wa Skauti Mkoa wa Dodoma Salama Katunda,akizungumza wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

AFISA wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Faustine Malecha,akitoa mada wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

MKUU wa shule ya Maria De Mathias,Lowael Lyimo,akielezea umuhimu wa TAKUKURU kuendelea kutoa semina kuhusu mapambana dhidi ya Rushwa nchini wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

AFISA Elimu Sekondari wa Jiji la Dodoma Bi.Upendo Rweyemamu,akizungumza wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina ya walimu walezi wa klabu za wapinga Rushwa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Maria De Mattias leo Machi 26,2022 Jijini Dodoma.

………………………………………………..

Na Alex Sonna, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kwa kuanzisha klabu za wapinga rushwa kwa Shule za Msingi na Sekondari huku akiwaasa walimu walezi wa
klabu kusimamia kwa weledi na kuelimisha wanafunzi namna ya kukabiliana na rushwa.

Mtaka ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua semina kwa walimu hao wa shule za msingi na sekondari jijini Dodoma.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kuhamasisha walimu kufanya kazi yao vizuri kwa kuwa klabu hizo ni moja ya njia ya kubadili mtazamo wa jamii ili vijana wakue wakiwa wazalendo, waadilifu wasiojihusisha na rushwa.

“Nishauri pamoja na kuwa na klabu za kupinga rushwa lakini pia TAKUKURU inaweza kutumia walimu wa dini ya kikristo na kiislamu shuleni kufundisha suala la rushwa vile vile, kwa kuwa wanafundisha kuhusu imani ni rahisi wanafunzi wengi kuelewa,”amesema.

Hata hivyo, amesema atashirikiana na taasisi hiyo kuandaa kongamano kubwa ambapo walimu walezi wa Mkoa mzima, baadhi ya wanafunzi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu wa Wilaya, Maafisa Elimu watashiriki kujadili madhara ya rushwa na hatua za kuchukua ili kujenga vijana waadilifu na wazalendo.

Ametaka taasisi hiyo iweke nguvu kubwa kwa klabu hizo ili kuwa na kizazi kinachotenda haki na hakijihusishi na rushwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa TAKUKURU, Sosthenes Kibwengo, amesema semina hiyo inalenga kuhamasisha na kuwafundisha walimu ili kuzisimamia vyema klabu kwenye shule zao.

“Pia kuhakikisha walimu wanakuwa chachu kwa klabu ili ziwe na tija na ziwe hai, klabu ni muhimu sana kwasababu vijana ndio wengi nchini ni karibu asilimia 62.4 ya wananchi wote, ni muhimu kuwashirikisha kwenye mapambano ya rushwa,”amesema.

Pia, ameshauri shule zote za Dodoma kutumia salamu ya ‘Rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea rushwa’ kabla ya kumsalimia mgeni anayefika shuleni kwao.

About the author

mzalendoeditor