Featured Kitaifa

TIC YASAINI MAKUBALIANO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA KIMKAKATI NA MAHIRI

Written by mzalendoeditor

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesaini makubaliano ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na Mahiri iliyochakatwa na kupitishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji yaani NISC baada ya kuridhishwa na kukidhi vigezo vilivyoainishwa na kamati hiyo.

Akishuhudia Utiaji wa Saini hizo hii leo Jijini Dodoma Naibu Waziri,Wizara ya Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud S.Kigahe amesema kuwa ushirikiano baina ya taasisi zilizo shughulikia masuala ya uwekezaji ni muhimu sana ili kuwaondolea usumbufu makapuni yanayotamani kuwekeze ndni ya nchi yetu.

Hivyo,umefika wakati wa kuondoa Ukiritimba na Urasimu usio na maana katika kushughulikia mikataba ya uwekezaji ili kumsadia muwekezaji kujua taratibu na wapi pakuanzia anapotaka kuanza mchakato wa kuwekeza.

“Niwaombe Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kushirikiana na taasisi zingine kuondoa huu ukiritimba na urasimu uliopo pamoja na kuondoa kabisa Vishoka au kuwarasimisha nao wawepo kisheria kwa sababu wanawasumbua sana wawekezaji mpaka wanakata tamaa ya kuwekeza nawaomba tena wathaminini na kuwajali watu na makampuni yanayotamani kuwekeza nchini kwetu msiwazungushe bila sababu za msingi kama mmepanga ni siku saba wapate huduma yao,” Amesema Mh.Exaud S.Kigahe

Pia amewataka kituo cha uwekezaji Tanzania Kutowapuuza na kuwagandamiza wawekezaji wa ndani kwani nao pia wanamchango mkubwa sana katika ukuzaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuzalisha ajira kwa Watanzania.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt.Madulu .I. Kazi amesema kuwa hadi kupatikana kwa makapuni hayo 6 kati ya 8 ambazo ziliomba Kuwekeza katika maeneo mbalimbali ni mchakato na mchujo mkubwa uliozingatia haki kwanzia kwenye vigezo na ubora.

Ambapo amebainisha kuwa uwekezeji huwa utasaidia kuinua zaidi uchumi wa taifa na kuchochochea maendeleo kwa wananchi kwani itazalisha ajira zaidi ya elfu ishirini na nane kwa watanzania.

Ameongeza kuwa malengo yao katika uwekezaji huo yalikuwa ni kuipunguzia serikali riba zinazotokana na kuagiza bidhaa nje ya nchi ndio maana wamelenga katika maeneo muhimu kama Sukari,Mafuta,Gasi na Madawa pamoja na Mbolea.

Miradi hiyo Sita ya kimkakati na Mahiri ambayo ni muhimu kwa nchi na inategemewa baada ya utekelezaji wake itakuwa na manufaa makubwa kwa taifa ambapo mradi wa kwanza ni mradi wa ltracom unaotekelezwa Mkoani Dodoma ,Mradi huu ni wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Mbolea na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 180 milioni na kuleta ajira zipatazo 4500 za moja kwa moja na 6,000 ambazo si za moja kwa moja. Mradi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani laki sita za mbolea kwa mwaka.

Na Mradi wapili ni wa Bagamoyo Sugar unaotekelezwa Mkoani Pwani ambapo Mradi huu ni wa Kilimo cha Miwa na Kiwanda kwa ajili ya uzalishaji wa sukari na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 193.75 milioni na kuleta ajira zipatazo 1500 za moja kwa moja na 10,000 ambazo si za moja kwa moja. Kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 300,000 za sukari na hivyo kupunguza mahitaji ya uagizwaji sukari kutoka nje.

Mradi wa Tatu ni wa Taifa Gas Unaotekelezwa nchi nzima ambapo Mradi huu ni wa uchakataji wa Gesi na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 62 milioni na kuleta ajira zipatazo 60 za moja kwa moja.

Na Mradi wa nne ni wa Kagera Sugar Unaotekelezwa Mkoani Kagera ambapo Mradi huu ni wa Kilimo cha Miwa na Kiwanda cha sukari na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 410 milioni na kuleta ajira zipatazo 10000 za moja kwa moja na 50,000 ambazo si za moja kwa moja. . Kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 300,000 za sukari na hivyo kupunguza mahitaji ya uagizwaji sukari kutoka nje.

Pia kuna Mradi wa Mtibwa Sugar Unaotekelezwa Mkoani Morogoro ambapo Mradi huu ni wa Kilimo cha Miwa na Kiwanda cha sukari na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani Milioni 150 na kuwa na jumla ya uwekezaji wa dola 305 Milioni na kuleta ajira zipatazo

12,500

Na Mradi wa sita ni wa Knauf unatekelezwa Mkoani Pwani ambapo Mradi huu unatekelezwa na Wawekezaji kutoka Ujerumani na utakuwa ni uzalishaji wa gypsum boards na gypsum powder na utakapokamilika unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 105 milioni na kuleta ajira zipatazo 150 za moja kwa moja na 500 ambazo si za moja kwa moja. Kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za mraba milioni 4

“Nchi yetu kwa sasa imefunguka na tunaamini kuwa mwaka huu tutaendelea kupokea wimbi kubwa la wawekezaji lakini pia tunajipanga kuboresha huduma zetu huku tukiwa tunafahamu umuhimu wa utekelezaji wa miradi hii ya kimkakati na mahiri,”Amesema Dkt.Madulu .I. Kazi

“Hivyo basi TIC, imejipanga kutoa huduma za haraka na kuhakikisha miradi yote inapata huduma ili mikataba hii itakayosainiwa leo iweze kutekelezwa,” ameongeza

TIC inaendelea na juhudi za kuunganisha mifumo ya serikali yaani dirisha la Pamoja la kuhudumia Wawekezaji la Kielektroniki Tanzania (Te/W)kwa taasisi zinazotoa huduma kwa wawekezaji kwani kwa kufanya maboresho hayo ya kuunganisha mifumo ni suluhisho la kuwawezesha na kurahisha upokeaji wa maombi, utoaji wa huduma za vibali, leseni na usajili kwa wawekezaji kwa haraka.

NAYE Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gas Tanzania Ltd Hamisi Ramadhani ameipongeza Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa uchaguzi bora uliozingatia vigezo na ubora na kuahidi kuwa watatekeleza kwa umahiri Mradi wao kwa sababu ndio matarajio ya kila Mtanzania ni kupata kilichobora na kuongeza kuwa kwa sasa sekta binafsi ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa.

About the author

mzalendoeditor