Watu watatu wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na nyati wakiwa shambani katika kijiji cha Mahurunga wilayani Mtwara.
Akithibitisha tukio hilo mbele ya waandishi wa habari leo Alhamisi Machi 24, 2022 Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo amewataja watu hao kuwa ni Rashid Bakari (40) mkazi wa kijiji cha Kitunguli, Salum Yusuf (46) na Said Musa (45) wakazi wa kijiji cha Mahurunga.
Amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 20 saa 5 asubuhi wakati watu hao wakiwa shambani ambapo walivamiwa na nyati na kuwashambulia.
“Baada ya kushambulia taarifa zilifika kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaolinda mpaka ambao walifika haraka na kumuua.” Amesema
Baada ya uchunguzi miili Ilichukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi.
Aidha, Kaimu Kamanda Katembo ametoa wito kwa wananchi akiwataka kutoa taarifa pindi wanapoona wanyamapori katika makazi ya watu.
Chanzo:Lango la habari