Featured Kitaifa

HATIMAE MZEE MREMA AFUNGA NDOA, MKE ASEMA ATAMRUDISHA UJANANI

Written by mzalendoeditor
IMG_20220324_133238

IMG_20220324_133241
IMG_20220324_133243IMG_20220324_133245

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Augustino Mrema leo Alhamisi Machi 24, 2022 amefunga ndoa na Doreen Kimbi katika kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mke wa mzee mrema anayejulikana kwa jina la Doreen Kimbi amesema kuwa atamrudisha mzee mrema ujanani.

“Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi. Katika kipindi cha uchumba nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata. Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana” amesema Doreen

Ameongeza kuwa hajafata mali kwa mzee mrema

“Mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake”

CHANZO:lango la habari

About the author

mzalendoeditor