Mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustino Mrema ametangaza kufunga ndoa siku ya Alhamisi Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha Mkoani Kilimanjaro.
.
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Parole Nchini anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Rose Mrema aliyefariki Dunia mwaka jana.
.
Mrema amesema amepata “binti mwenye umri mdogo” mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari.
.
Amesema kilicho msukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa maisha yake kwani yeye ni mzee na anahitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu huku akiishukuru familia yake kwa kumkubalia.
.