Na Alex Sonna
LICHA ya Simba kupoteza kwa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya wenyeji ASEC Mimosas Kipa Aisha Manula ameibuka shujaa kwa kudaka Penalti mbili na kunusuru kulala kwa mabao matano katika Mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa nchini Benin.
Mabao ya wenyeji yamefungwa na Aubin Kramo dakika ya 16,Stephane Aziz Ki dakika ya 25 na Karim Konate dakika ya 57 huku wakikosa Penalti mbili zilizopigwa na Stephane Aziz Ki pamoja na Karim Konate.
Kwa ushindi huo ASEC Mimosas wamefikisha Pointi 9 na kuongoza kundi hilo huku Simba akishuka nafasi ya tatu akiwa na Pointi 7 akiwa sawa na RSB Berkane na US Gendarmerie wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na Pointi 5.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo US Gendarmerie wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na RSB Berkane .
Simba bado wa nafasi ya kutinga robo fainali mchezo wao wa mwisho watacheza uwanja wa Benjamin Mkapa watakapocheza na US Gendarmerie huku ASEC Mimosas watamalizia ugenini nchini Morocco kucheza na RSB Berkane.