Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YANYOOSHEA KIDOLE UJENZI WA HOSPITALI MBARALI

Written by mzalendoeditor

OR- TAMISEMI

Mwenyekiti wa Kamati  ya   Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Grace Tendega amesema Hawajaridhishwa  na    matumizi ya fedha katika ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya   katika  Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Mhe. Tendega amesema kuwa gharama iliyotumika katika utekelezaji wa ujenzi ni kubwa ukilinganisha na  majengo ambayo yamejengwa, pia  majengo ambayo yamekamilika hayana viwango  huku mengine yakihitaji ukarabati hata kabla hayajaanza kutumika.

Kauli hiyo imetolewa Machi 18, 2022 katika ziara ya Kamati ya   Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ilipotembea na  kukagua ufanisi wa utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Mbarali.

“Ujenzi wa hopitali ya Mbarali hatujaturidhisha kabisa,gharama iliyotumika    imetupa wasiwasi mkubwa haiendani na uhalisia, pili  majengo hayana ubora unakuta mengine kuta zina nyufa” Amesema Mhe. Tendega.

Ameongeza kuwa dhana ya kutumia force account katika utekelezaji wa miradi ni kupunguza gharama kwa   kuzingatia ubora katika utekelezaji lakini, ameshangazwa  na gharama kubwa ambayo imetumika   katika ujenzi huo ilhali umetekelezwa kupitia force account.

Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa ,Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt.Switbert Mukama ameihakikishia Kamati kuwa itatekeleza maagizo yaliyotewa na Kamati kuhusu ujenzi wa hospotali hiyo.

Katika hospitali hiyo majengo yaliyokalimika ni   jengo la utawala na wagonjwa wanje, jengo la dawa, jengo la kufulia nguo, jengo la chanjo, jengo la jenereta pamoja na jengo la mionzi, jengo la maabara, wodi ya wazazi , wodi ya watoto, wodi ya wanaume na wanawake yapo katika hatua ya umaliziaji.

About the author

mzalendoeditor