Featured Kitaifa

NAIBU KATIBU MKUU MADINI AKAGUA KITUO CHA UMAHIRI MPANDA-KATAVI

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameendelea na ziara yake ya kutembelea shughuli za madini katika maeneo mbalimbali nchini ambapo amekagua Jengo la Kituo cha Umahiri Mpanda, Mkoa wa Katavi.

Pamoja na kukagua kituo hicho pia, amezungumza na watumishi na kuwataka kuendelea kubuni mikakati itakayoendeleza kukuza makusanyo ya maduhuli ya Serikali ikiwemo kutumia vema fursa ya miradi mikubwa ya ujenzi kama barabara nakadhalika ili kuongeza makusanyo kupitia madini ujenzi sambamba na madini mengine.

Pia, ameendelea kusisitiza suala la uadilifu na bidii katika kazi ambapo pia amewakumbusha watumishi kuhusu umuhimu wa Sekta ya Madini katika kuchangia ustawi na maendeleo ya watanzania na hivyo kuwataka kutambua dhamana kubwa waliyopewa na kuwataka kutenda haki.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Katavi, Paul Hilbaqambaway ameahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yanayotolewa kwa ajili ya maendeleo ya sekta.

Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu ameambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wizara ya madini, Issa Nchasi.

About the author

mzalendoeditor