HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, inatarajia kuanzisha benki ya maziwa ya binadamu.
Akizungumza leo Ijumaa Machi 18, wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo, Naibu Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Julieth Magandi, amesema uanzishaji wa benki hiyo utasaidia watoto ambao mama zao wana changamoto.
“Tuna mpango wa kuanzisha benki ya maziwa ya binadamu, ili watoto wanaozaliwa na mama zao hawana maziwa au kuwa na changamoto wanapatiwa maziwa hayo.
Dk. Mgandi amesema tayari wameshafanya tathmini na wananchi wako tayari kuchangia maziwa.
Chanzo:Global Tv