Jengo la kituo jumuishi la utoaji haki kanda ya Arusha.
Picha ya pamoja ya kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na sheria pamoja naibu waziri wa Katiba na Sheria Geoffrey Pinda, Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Mzuna na baadhi ya watendaji wa mahakama kuu ya Tanzania.
Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria Emmanuel Mwakasaka akiongea wakati walipotembelea kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Noah Lemburis Saputu akiongea walipotembelea kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Mahonda Kaskazini Unguja Abdullah Ali Mwinyi akiongea kamati hiyo ilipotembelea kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Mbunge viti maalum upande wa watu wenye mahitaji maalum mkoa wa Dodoma Khadija Shabani.
Naibu waziri wa Katiba na Sheria Geoffrey Pinda akiongea na kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Ni kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria wakitembelea baadhi ya maeneo katika jengo la kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria imeishauri mahakama ya Tanzania kutunza miundombinu iliyokwa katika vituo jumuishi vya utoaji haki nchini ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo yanapita katika televisheni zilizowekwa katika kuta za mahakama hizo juu ya kesi kwa lugha ya kiswahili ili wananchi waweze kuelewa.
Aidha kamati hiyo imedhizishwa na ujenzi wa miundombinu katika vituo hivyo vilivyojengwa kwa ustadi na kuweza kuyafikia makundi yote, ikiwemo tasisi zinazojishughulisha na haki za binadamu, mawakili wa kujitegemea, watu wenye walemavu, wanawake wanaonyosha, watoto pamoja na tasisi nyingine za serikali.
Mbunge viti maalum upande wa watu wenye mahitaji maalum mkoa wa Dodoma Khadija Shabani aliipongeza mahakama hiyo kwani haiokoi muda tuu bali ni pamoja na fedha ambazo wananchi wangezitumia kutoka mahakama moja kwenda nyingine na hayo ndio maendeleo wanayoyataka.
Abdulla Ali Mwinyi mbunge wa Jimbo la Mahonda Kaskazini Unguja alisema kuwa ameridhishwa na miundombinu iliyowekwa katika mahakama hiyo kwani ni ya kiwango cha kimataifa lakini pamoja na kuwa na kiwango hicho ina sura ya Tanzania kwa kutumia majina na vifaa vya vinavyotengenezwa hapa nchini.
Suma Ikenda Fyandombo mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya aliipongeza mahakama hiyo kwa kuona umuhimu wa kuweka chumba maalum Cha kunyonyeshea watoto kwani utamaduni huo unatumika kimataifa lakini pia kwa kutengeneza maeneo maalum kwaajili ya watoto wanaokabiliwa na kesi pamoja na wanaotoa ushahidi katika kesi zinazoendelea.
Eduward Ole Kaita mbunge wa Jimbo la Kiteto alisema kutokana na ubora wa majengo ya mahakama ya Tanzania ili ilete matokeo ya miundombinu hiyo ni vema watanzania wapate haki zaidi inayoendana na ubora huo lakini pia aliishahauri mahakama kuwa matangazo yanayotolewa katika televisheni zilizopandikwa katika kuta kuhusiana na kesi zinazoendelea katika majengo hayo yatolewe kwa lugha ya kiswahili ili kusaidia wananchi kuelewa kwa haraka.
Joseph Anania Thadayo mbunge wa Jimbo la Mwanga alisema kuwa mahakama ni moja kati ya mihimili ambayo haina jukwaa la kusemea mambo yake na kwa kuzingatia Kuna watu wachache ambao wanaitangaza Tanzania vibaya kuwa haina demokrasia ambapo mabosesho yaliyofanyika yanapaswa kutangazwa kwani hata tasisi mbalimbali zinazoshighulika na masuala ya haki za binadamu kwasasa wamekuwa sehemu ya mahakama.
“Nchi ambayo haina demokrasia wala utoaji wa haki haiwezi kuwekeza fadha nyingi hivi katika kuboresha miundombinu ya mihimili huu ambao ndio kiini cha utoaji wa haki,” akisoma Thadayo.
Noah Lemburis Saputu mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi aliishahuru mahakama ya Tanzania kutoa kipaumbele cha ujenzi katika maeneo ambayo wameyakodisha.
Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka alisema kuwa wao wakiona dosari wanaisema, hawawezi kufumbia macho kwani ndio majukumu yao waliyokabidhiwa kwa niaba ya wabunge wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika tasnia hiyo ya katiba na sheria lakini wameridhika na kazi ya utendaji wa mahakama hiyo na mamna ambayo hawamuangushi Mh. Rais Samia Suluhu katika utendaji wao wa kuisimamia tasnia hiyo.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Katiba na Sheria Geoffrey Pinda alisema kuwa anashukuru kwa kuwa kile ambacho walikitarajia wameweza kuona kwa macho na wanapotekeleza wajibu wao nje ya kuangalia watu wengine bado wanawaangalia kamati na wabunge wote kwani ndio wanawapitishia fedha hizo zilizotumika katika ujenzi.
“Nampongeza sana Rais Samia ambaye ndiye mwezeshaji wa haya yote na kwasasa vituo jumuishi vya utoaji haki vipo 6 na tunategemea kuanzisha vingine ili kuwapunguzia watanzania adha ya kutumia gharama kubwa pale watakapohitaji kupata huduma hii,” Alisema Pinda.
Kwa upande wake Profesa Elisante ole Gabriel Mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania alisema kuwa wanalengo la kujenga vituo jumuishi vya utoaji haki 12 pamoja na mahakama za mwanzo 60 ambapo kwa Sasa mahakama hizo ambazo ziko sita nchini.
Alifafanua kuwa manufaa ya mahakama hiyo ni pamoja na kuongeza imani ya mahakama kwa wananchi, inaokoa muda kutokana na mahakama zote kuwepo eneo hilo, inaepusha mrundikano,pamoja na kuongeza hari ya utendaji.
Hata hivyo vituo hivyo vimejengwa katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Dodoma, Mwanza na mkoa wa Dar es salaam katika wilaya ya Kinondoni na Temekea ambapo kila moja imegharimu shilingi bilioni 8 na katika kuhakiki thamani ya fedha wamefanikiwa kuokoa zaidi ya bilioni 3.