KAMATI ya siasa ya mkoa wa Arusha pamoja na wilaya ya Meru wakikagua eneo lililoanza kujengwa msingi kwaajili ya jengo la mama na Mtoto katika kituo cha Maroroni kinachojengwa kwa kutumia fedha za ndani za Halmashauri.
KAMATI ya siasa mkoa wa Arusha na wilaya ya Meru wakikagua ujenzi wa kituo cha afya katika KATA ya Maroroni kinachojengwa kwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.
MJUMBEwa kamati ya siasa mkoa wa Arusha Robert Paul Kaseko akiongea katika jengo la zahanati inayoendelea kujengwa katika kata ya Kikatiti.
MKURUGENZI
wa halmashauri ya Meru Mwalimu Zainabu Makwinya akielezea jambo katika zahanati ya Kikatiti inayoendelea na ujenzi.
KAMATI ya siasa mkoa na wilaya wakiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwalimu Zainabu Makwinya wakati wakikagua ujenzi wa zahanati ya Kikatiti.
MJUMBE wa kamati ya siasa wilaya ya Meru Mathayo Leiya Mafie akiongea wakati wakikagua ujenzi wa zahanati ya Kikatiti.
…………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha na wilaya ya Meru imeshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuunga mkono ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kikatiti uliodumu kwanzia 2013 huku wakimshukuru kwa kuwapa mkurugenzi wa halmashauri ya Meru anayejali maslahi ya wananchi Mwl Zainabu Makwinya.
Akiongea katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayoendelea katika halmashauri hiyo mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Arusha Robert Paul Kaseko alisema kuwa Mh. Rais kwa kuguswa na shida za wananchi alichangia milioni kumi katika ujenzi wa zahanati hiyo October 2021 lakini amewapa mkurugenzi ambaye ana msukumo mkubwa wa shughuli za kiutendaji hasa katika kufuatilia na kusimamia miradi ya serikali inayotekelezwa katika halmashauri hiyo.
“Madiwani na viongozi wengine wote mkimtumia vizuri Mwalimu Zainabu 2025 wapinzani hawatakuwa na la kusema kwani ni mtu ambaye anajibidiisha mwenyewe na anajua namna na wapi pa kutafuta rasilimali fedha kwaajili ya kuwanufaisha wananchi, angoji fedha zinazotoka serikalini tu peke yake na kama mnavyoona ndani ya muda mfupi ametafuta mdau ambaye endapo mambo yatakaa vizuri atamalizia kituo hicho,” Alisema
Alifafanua kuwa kituo hicho ambacho ujenzi ulisimama kutokana na rasilimali fedha ndani ya muda mfupi wameshaonyesha fedha ambazo alizitoa Rais Samia milioni 10 na halmashauri milioni 10 huku mbunge naye akichangia milioni tano ambazo zinaweza kuingia muda wowote mpaka hapo wameona zahanati hiyo inaenda kukamilika.
Mjumbe wa Kamati ya siasa wilaya hiyo Mathayo Leiya Mafie alisema kuwa tangu kuanza kwa mradi huo 2013 mkurugenzi huyo ni wakwanza kutoa mkazo katika ujenzi huo na amekuwa sehemu ya Kikatiti yeye pamoja na mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na mhandisi.
“Wao kuwepo mara kwa mara mahali hapa wanaendelea kuona ni changamoto gani zipo na juzi amekuja na mdau ambaye amekubali kutusaidia kwahiyo anafanya kazi nzuri ambayo inaonyesha haikuwa makosa yeye kuja Meru lakini pia anakipa heshima chama cha mapinduzi ambapo 2024/2025 wapinzani watakuwa hawana hoja tena kwani hoja yao ilikuwa Zahanati hii,” Alisema Mafie.
“Mkurugenzi umesema hata wadau wengine umeongea nao endelea kupambana nao angalau kituo hiki kikamilike na mbele ya safari ikiwezekana kiwe kituo cha afya,”alieleza.
Diwani wa kata ya Kikatiti Kisali Majala alieleza kuwa kuwa milioni 10 alizitoa Rais Samia ndio zimekuwa kichocheo cha kuendeleza ujenzi wa zahanati hiyo lakini pia ushirikiano wa mkurugenzi ambaye anafanya kazi hiyo kama ya kwake kwa kujituma muda wote anaamini atamalizia ujenzi huo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Meru Mwalimu Zainabu Makwinya alisema kuwa ameandika barua kwaajili ya kuwaomba wadau mbalimbali waeasaidie ili waweze kukikamisha kwani Mh Rais ametoa hizo milioni 10 sio kwamba hana fedha ila anataka aone na wao kama wanaweza hivyo ameanza kutafuta wadau na kuna mmoja alishafika katika eneo hilo na wameshamtengenezea bajeti.
Naye mtendaji wa kijiji cha Kikatiti Abel Kaaya alisema kuwa kwasasa zinahitajika zaidi ya milioni 200 ili kukamilika kwa Zahanati hiyo ambapo hadi hapo ilipofikia zimeshatumika zaidi ya milioni 90 ikiwemo milioni 70 inayochangwa na wananchi, milioni tano kutoka mfuko wa Jimbo, milioni 10 alizitoa Rais Samia October 16,2021 pamoja na milioni 10 iliyotolewa na halmashauri.
Sambamba na hayo pia kamati hiyo iliweza kukagua ujenzi kituo cha afya pamoja na jengo la mama na mtoto katika kata ya Maroroni inayojengwa kwa fedha za ndani za halmashauri hiyo pamoja ukaguzi wa madarasa ya katika shule ya sekondari Kiwawa, Embaseni pamoja na Shambarai Burka.