Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akiongoza Mkutano wa Baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha tarehe 14 Machi, 2022.

………………………………………………………………..

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamekumbushwa kuzingatia maadili wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Wito huo umetolewa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili  ya Viongozi wa Umma lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa IACC jijini Arusha tarehe 14 Machi, 2021.

Mhe. Mwangesi alisema kuwa jukumu kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma, hivyo basi ni muhimu kwa watumishi wa Taasisi wakazingatia maadili na kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa umma katika Nyanja ya Uadilifu.

 “Ninawaasa kwa mara nyingine kwa kuwa tumekubali kuwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma hatuna namna zaidi ya kuzingatia nidhamu, kuwa waaminifu na kupendana; atakayeenda tofauti na hayo atakuwa ameamua kuwa si miongoni mwetu na hatutasita kulichukulia hatua suala la namna hiyo”. Alisisitiza Mhe. Mwangesi.

Mhe. Mwangesi aliendelea kufafanua kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo katika kazi yao ya kusimamia uadilifu, aliwaomba watumishi hao wasikubali kuyumba au kuyumbishwa na hatimaye kutolewa kwenye mstari na badala yake waendelee kufuata misingi ya Weledi na Maadili katika utendaji kazi kwa kuepukana na rushwa na kushinda vishawishi vya rushwa na tamaa nyinginezo.

Akizungumzia lengo mahsusi la Mkutano huo alisema kuwa ni kupokea taarifa ya mapitio ya bajeti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 na mwelekeo wa bajeti kwa mwaka 2022/2023.

“Ninatambua kuwa katika Taasisi yetu tuna mahitaji mengi na ya msingi na yote yanahitaji uwepo wa fedha.  Kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali, ninaomba mipango na majadiliano yetu kuhusiana na bajeti ya mwaka 2022/2023 vizingatie vipaumbele vya Taasisi yetu pamoja na kazi zinazoonekana na kupimika”.Aliendelea kufafanua Mhe. Mwangesi.

Kwa upande mwinge, Mhe. Mwangesi alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuchukua tahadhali dhidi ya mlipuko wa homa ya mafua makali (UVIKO 19) kwa kuwaasa watumishi hao kuendelea kusikiliza na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa masuala ya afya kuhusiana na namna bora ya kujikinga dhidi ya mlipuko huo.

Previous articleNYWELE NA NYUSI ZA BINTI ZAGOMA KUOTA MIAKA 23 SASA BAADA YA KUNYOLEWA NA BABA YAKE
Next articleKAMATI YA PAC YAKAGUA MRADI WA KUUNGANISHA UMEME KENYA NA TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here