Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MRADI WA MAZINGIRA KONDOA, DODOMA

Written by mzalendoeditor

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua shughuli za kilimo msitu ya alizeti katika shamba darasa lililopo Kijiji cha Haubi Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022, kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. David Kihenzile akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo kujionea shughuli ya utengaji wa msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi wilayani Kondoa mkoani Dodoma chini ya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ziara iliyofanyika leo Machi 12, 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis akifafanua jambo kuhusu taarifa ya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira leo Machi 12, 2022 wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli ya utengaji wa msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi wilayani Kondoa mkoani Dodoma chini ya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ziara iliyofanyika leo Machi 12, 2022.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

About the author

mzalendoeditor