Featured Kitaifa

CCM YAIAGIZA SERIKALI KUANGALIA UPYA MWENENDO WA JESHI LA POLISI NCHINI

Written by mzalendoeditor

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hamidu Shaka amesema kuwa Kamati kuu ya Halmashauri kuu Taifa ya chama hicho imeielekeza Serikali kuangalia upya Mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi kutoka na matendo yanayofanywa na baadhi ya maafisa na askari  kinyume na miongozo wa utendaji kazi wa jeshi hilo.

Shaka amesema hayo leo Machi 12,2022 akizungumza na waandishi wa Habari akitoa taarifa kwa umma kuhusu kikao cha Kamati ya chama hicho iliyoketi jana  chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Hassan.

About the author

mzalendoeditor