PROFESA George Wajackoyah; ni mmoja wa wagombea urais nchini Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, mwaka huu ambaye ameahidi kuruhusu bangi nchini humo kama akipata Urais huo.

Profesa Wajackoyah akiwa kwenye kampeni zake kwa Wakenya Wanaoishi Nchini Marekani, ameliambia Shirika la Habari la Sauti ya Amerika (VOA) kuwa, endapo akipata kiti hicho ataruhusu biashara ya bangi ili mapato yatokanayo na mauzo ya zao hilo yalisaidie Taifa hilo kumaliza kulipa mikopo mikubwa ya kimataifa inayodaiwa.

“Kenya tuna madeni makubwa ya Wachina, iwapo tutalima bangi tutapata pesa za kuwaondoa Wachina nchini kwetu.

“Gunia moja la bangi ni karibu Dola Milioni 3, iwapo tukilima hekta elfu 10 nchi inaweza kuzalisha bangi ambayo huwa inachukua miezi 6 kisha tunayauzia mataifa makubwa ili kulipa madeni ya Wachina kwa sababu mambo wanayofanya Kenya kutaifisha mali siyo ya halali,” Wajackoyah ameiambia VOA

Previous articleCCM YAIAGIZA SERIKALI KUANGALIA UPYA MWENENDO WA JESHI LA POLISI NCHINI
Next articleBASHUNGWA ATAKA WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA KWA MTAKA UJENZI WA SOKO LA MACHINGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here