Rais Vladimir Putin wa Urusi ametoa idhini kwa watu wa kujitolea kutoka Mashariki ya Kati kwa ajili ya kupigania Urusi mashariki mwa Ukraine.

Waziri wa Ulinzi, Sergei Shoigu amesema kuna watu 16,000 wa kujitolea katika Mashariki ya Kati ambao walikuwa tayari kuja Donbas.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na uvumi kwamba wanajeshi wa serikali ya Syria walio na vita kali wanaweza kulipwa na Urusi kupigana huko Ukraine.

Jeshi la anga la Urusi na baadhi ya vitengo maalumu vimekuwa na jukumu muhimu kumuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Previous articleMBUNGE WA HAI ATANGAZA KUMALIZA CHUKI NA MWENYEKITI WA CHADEMA
Next articleMKURUNGEZI MTENDAJI IMF AITAHADHARISHA AFRIKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here