Featured Kimataifa

MKURUNGEZI MTENDAJI IMF AITAHADHARISHA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Kristalina Georgieva, jana Machi 10, 2022 amekutana na mawaziri wa fedha wa mataifa ya Afrika, kujadili athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Akizungumza katika makao makuu ya shirika hilo mjini Washington Dc, Marekani amesema mtazamo wa kiuchumi wa Afrika uko katika hatari ya kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta kutokana na vita hivyo.

Mataifa ya Afrika pia yapo katika atharu ya kupungua kwa mapato yatokanayo ya utalii na kupungua kwa upatikanaji wa huduma za kifedha.

Georgieva amesema nchi nyingi zitalazimika kurekebisha sera zake, na kuongeza kuwa IMF iko tayari kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza gharama za marekebisho yoyote ya kisera.

About the author

mzalendoeditor