Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akisoma barua ya malalamiko iliyoandikwa kwenye ofisi ya Rais na wananchi wakiomba serikali kuwapatia ufumbuzi wa maeneo yao waliyodai kuporwa na kupigwa mnada.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bahi kata ya Mpamantwa jana 7 Machi 2022 kwenye kikao kilichofanyika kijijini hapo kwa lengo la kutatua mzozo wa ardhi uliopo baina ya vijiji hivyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda akizungumza na wanakijiji wa kata ya Mpamantwa na Bahi Sokoni kwenye kikao kilichofanyika jana 7 Machi 2022 kilicholenga kutatua mzozo wa ardhi uliopo baina ya vijiji hivyo.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye kikao hicho na kutoa malalamiko yao mbele ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

…………………………………………………………

Na Bolgas Odilo-DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka amewataka wanakijiji wa kata ya Mpamantwa na Bahi Sokoni Wilayani Bahi kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kupata maeneo yao wanayodai kuwa waliporwa na kupigwa mnada na viongozi wao.

Mhe. Mtaka  kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mpamantwa kata ya Mpamantwa uliokua na lengo la kusikiliza a kutatua malalamiko yaliyotolewa kwa njia ya maandishi (barua) moja kwa moja kwenye ofisi ya Rais.

Akijibu hoja hiyo, Mtaka aliwataka wananchi wanaodai kuporwa maeneo yao kuwa wavumilivu kwa kipindi ambacho uongozi wa wilaya unafanya tathmini ya kubaini idadi kamili ya wananchi wenye viwanja katika maeneo yenye mzozo na kuwahakikishia kila mmoja atapata haki yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kufika na kuzungumza na wananchi hao na amekua mstari wa mbele katika kutatua kero mbalimbali za wananchi mkoani humo.

Munkunda alisema kuwa, ameyapokea maelekezo aliyopewa na mkuu wa mkoa na atayafanyia kwa uharaka zaidi ili kuhakikisha wanakijiji hao wanapata haki zao kama inavyostahiri ili kusiendelee kuwepo kwa hali hiyo ingawa kabla walishazungumza na wanakijiji hao.

Aidha, akifunga mkutano huo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka alisema kuwa, hakuna sababu ya wananchi hao kuishi kwa chuki baina yao kwani tayari suala hilo limeshafika kwenye uongozi mkuu hivyo wawe wavumilivu wakati serikali inatafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Kwa upande wa wakazi wa maeneo hayo wameoneshwa kuridhishwa na uamuzi wa Mkuu wa Mkoa na kuwa wako tayari kusubiri ili waweze kupatiwa haki zao.

Previous articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MARCH 9,2022
Next articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI JUKWAA LA UCHUMI DUNIANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here