Featured Kitaifa

MBUNGE KATAMBI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM JIMBO LA SHINYANGA MJINI

Written by mzalendoeditor

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini walipokutana katika Kata ya Old Shinyanga Machi 7, 2022.

Sehemu ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini wakisikiliza maelezo ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb) walipokutana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika Mkoa huo

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Bw. Abubakari Mkadam (kulia) akieleza jambo wakati wa mkutao huo. Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb). Kushoto ni Mwenyekiti wa Kata ya Lubaga, Bw. Anord Makombe.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Bi. Agnes Bashem akizungumza katika mkutano huo ulioongozwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika Mkoa huo.

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata za Mwamalili, Chibe, Old Shinyanga na Lubanga wakifuatilia mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb) akisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata za Mwamalili, Chibe, Old Shinyanga na Lubanga wakati wa mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Bw. Abubakari Mkadam.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Bw. Abubakari Mkadam wakati wa Mkutano huo.

Diwani Viti Maalum kutoka Tarafa ya Shinyanga mjini, Bi. Paschazia Semi (kushoto) akitoa neno la shukuran kwa Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo la Shinyanga Mjini kwa kufanikisha maendeleo ya miradi mbalimbali. Kulia ni Diwani Kata ya Lubaga, Bw. Ruben Dotto.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb) akiwa ameambatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Bi. Ester Makune (kulia) pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipotembelea na kukagua Daraja la Upongoji lilojengwa kwa fedha za maendeleo ya Jimbo.

Muonekano wa Daraja la Upongoji lililojengwa kwa fedha za maendeleo ya Jimbo kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb).

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb) akikagua Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ndala alipowasili katika soko lililopo eneo la Ndala kwa lengo la kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM katika Kata ya Kambalage, Ndala, Masekelo na Mwawaza.

 

PICHA NA OFISI YA MBUNGE

(JIMBO LA SHINYANGA MJINI)

About the author

mzalendoeditor