Featured Michezo

WACHEZAJI WATATU TEGEMEO SIMBA KUWAKOSA BIASHARA UNITED

Written by mzalendoeditor

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amethibitisha kukosa huduma ya nyota wake watatu kwenye mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Biashara United utakaopigwa kwenye uwanja wa Benajamin MKapa majira ya saa 1:00 usiku.
 
Pablo amesema atawakosa kipa Aishi Manula ambaye ana matatizo ya kifamilia, Sadio Kanoute (majeraha) na Taddeo Lwanga ambaye bado hajawa fiti.
 
 “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Biashara baada ya kumaliza majukumu yetu kwenye mechi za kimataifa, tutaingia kwenye mchezo huu kwa kuwaheshimu kwani wamekuwa na mchezo mzuri dhidi ya timu kubwa ukizingatia walifanikiwa kutuzuia kwenye raundi ya kwanza.

Vijana wapo tayari kwa ajili ya mchezo isipokuwa tutawakosa Aishi Manula ambaye amepata matatizo ya kifamilia, Sadio Kanoute alipata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Berkane na Taddeo Lwanga ambaye bado hajawa fiti.”

About the author

mzalendoeditor