Featured Kitaifa

HAKUNA FARU MWEUSI ALIYEONEKANA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA NYERERE

Written by mzalendoeditor

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taarifa iliyotolewa na mtandao wa Tanzania Times tarehe 3 Machi, 2022 ikieleza kuonekana kwa faru mweusi katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Taarifa hiyo ambayo inaendelea kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii sio sahihi na tunaomba ipuuzwe. Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo.

Aidha, Wizara inasisitiza kuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya wanyampori hapa nchni ikiwemo utoaji wa takwimu na taarifa za wanyamapori kwa umma ni Wizara ya Maliasili na Utalii na si vinginevyo.   

About the author

mzalendoeditor