Kituo cha Mtambo mkubwa wa Nishati ya Nyuklia Barani Ulaya kilichoko Ukraine kimelengwa katika mashambulizi ya Urusi usiku wa kuamkia leo Ijumaa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba ametaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo ili kuepusha Maafa
Msemaji wa Mtambo huo wa Zaporizhia , Andrei Tuz amesema shambulio la makombora lililofanywa na Vikosi vya Urusi, limesababisha Moto kuwaka katika mojawapo ya sehemu ya kituo hicho