Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo, kuingia kwenye ukumbi wa TANAPA jijini Arusha kwa ajili ya  ufunguzi wa mkutano  wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika,  Februari 28, 2022.  Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano huo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo (wa nne kushoto) na Rais wa Mahakama ya Afrika, Imani Aboud( wa tano kushoto) wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Wa pili kulia ni Waziri wa katiba na Sheria, George Simabachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Wengine pichani ni Majaji wa Mahakama hiyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea nembo ya Mahakama ya Afrika kutoka kwa Rais wa Mahakama hiyo Imani Aboud, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono na kuimarisha ushirikiano uliopo na Umoja wa Afrika hasa katika kuzingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 28, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Mkutano huo unafanyika jijini Arusha.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kwama Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapokea na kushirikiana nao pale watakapohitaji ushauri wa aina yoyote. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.

Amesema Mahakama hiyo ilianzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kusimamia haki za binadamu, ambapo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia alipata fursa ya kueleza dhamira ya Tanzania katika kuunga mkono jitihada za mahakama hiyo kufanya kazi.

Naye, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo akizungumzia kuhusu ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika inayolenga kulifanya Bara la Afrika kuwa bara lenye nguvu duniani katika siku zijazo amesema kuwa ipo haja ya kutambua changamoto zinazokabili Bara la Afrika ili waifikie Afrika wanayoitaka.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuangalia namna ya kutafsri yote yaliyoanishwa kwenye agenda 2063. “Lazima tutumie fursa na taasisi zote tulizonazo ili tuweze kufikia Afrika tunayoitaka lengo ni kuhakikisha tunaona maisha ya Waafrika yanaboreshwa na uchumi unakua.”

Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wanaoupata ambapo unawawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. 

Previous articleRAIS SAMIA AREJEA NCHINI MARA BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI KATIKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE)
Next articleBILIONI 27 ZATOLEWA KUBORESHA BARABARA ZA RUKWA- RC MKIRIKITI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here