Featured Michezo

MMILIKI WA CHELSEA ABRAMOVICH AJIUZULU

Written by mzalendoeditor

Mmiliki wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich ametangaza kujiuzulu ndani ya Klabu hiyo. Kujiuzulu kwake kunamaanisha amejitoa kwenye uongozi wa bodi ya klabu hivyo hatokuwa mtu wa mwisho kutoa tamko na maamuzi ya mwisho kama ilivyokuwa hapo awali.

Abramovich amefikia hatua hiyo baada ya kuongezeka kwa ghasia nchini Ukraine, hali iliyopelekea Urusi kuwekewa vikwazo kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo Uingereza dhidi ya Urusi.

Majukumu aliyokuwa akiyafanya Abramovich ameyaacha kwenye uongozi wa bodi ambao unaongozwa na Marina Granovskaia pamoja na rais wa Chelsea, Bruce Buck.

Abramovich hajauza klabu au kujitoa kabisa ndani ya Chelsea badala yake anabaki kuwa mmiliki wa klabu lakini hatokuwa na sauti ya mwisho kwenye kufanya maamuzi.

About the author

mzalendoeditor